Jumapili, 15 Septemba 2013

SUNDERLAND 1 ARSENAL 3




Aaron Ramsey aliifungia Arsenal Bao 2 walipoitandika Sunderland Bao 3-1 huko Stadium of Light.
Mchezaji mpya wa Arsenal, Mesut Ozil, ambae alicheza vizuri, ndie aliempa pasi Olivier Giroud kufunga Bao la Dakika ya 11 lakini Sunderland walisawazisha kwa Bao la Penati ya Craig Gardner katika Kipindi cha Pili.
Lakini baada ya Ramsey kufunga Bao la Pili kwa Arsenal, Refa Martin Atkinson alileta utata mkubwa pale Jozy Altidore alipomtoka Bacary Sagna na kufunga Bao lakini Refa huyo aliashiria kuwa Sagna alicheza Faulo kabla Bao kufungwa na kuwaacha Sunderland wakilalamika kwanini Bao halikubaki.
Hata hivyo, Ramsey akafunga Bao la 3 na kuwanyamazisha Sunderland na kuipa Arsenal ushindi wa Bao 3-1.
VIKOSI:
Sunderland: Westwood, Celustka, Diakite, Roberge, Colback, Johnson, Ki, Vaughan, Mavrias, Altidore, Fletcher
Akiba: Brown, Larsson, Gardner, Wickham, Cuellar, Mannone, Borini.
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Koscielny, Gibbs, Wilshere, Flamini, Ozil, Walcott, Giroud, Ramsey
Akiba: Vermaelen, Monreal, Fabianski, Frimpong, Miyaichi, Gnabry, Akpom.
Refa: Martin Atkinson

Hakuna maoni: