Fujo zaanza: Maofisa wa polisi wameshindwa kuwazuia
maelfu ya watu katika mapokezi hayoNa Baraka Mpenja kwa msaada wa
Sportsmail.com
Nyota wa zamani wa Manchester United, Los Angel
Galaxy, Real Madrid, PSG na timu ya taifa ya England,
David Beckham amewasili leo nchini China na kusababisha wanafunzi watano
kujeruhiwa vibaya katika harakati za kumpokea katika chuo cha Tongji
University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
Beckham ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira
wa miguu ya chuo hicho kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye
lengo la kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono
na nyota huyo, imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha
watu kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa
kutimia kufuaia fujo hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika
mtandao wake wa kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile
kilichotokea.
Samahani sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo
kikuu pale uwanjani, kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia
watu wachache wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri
wapone salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo
na kuhitaji kumshika nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa
maofisa wake watu wamejeruhiwa katika fujo zoezi hilo.
Beckham mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka
msimu uliopita ambapo aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini
Ufaransa, Ligue 1




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni