Jumanne, 23 Aprili 2013

Ungekuwa wewe ungemfanya nini mlevi huyu..!!




Jamaa alikuwa amelala na mkewe saa tisa ya usiku wakaamshwa na mtu akipiga hodi mlangoni kwao. Wakabishana nani akafungue hatimae mume akaenda na kufungua mlango. Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
MUME: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia
MLEVI: Okay nisukume basi..
Wewe ungemfanyanini  mlevi huyu?

Hakuna maoni: